Kwa Uchapishaji wa Mara Moja
Mawasiliano: Cynthia Santana/Meneja Mawasiliano
206-256-5219
cynthia.santana@seattle.gov
Ofisi ya Viwango vya Kazi (Office of Labor Standards) Imetangaza Kiwango cha Chini cha Mshahara cha Seattle Kwa 2026
Seattle, WA – (Septemba 30, 2025) – Ofisi ya Viwango vya Kazi ya Seattle (OLS) imetangaza ongezeko la kiwango cha chini cha mshahara Seattle, kitakachoanza kutumika Januari 1, 2026. Ongezeko la kila mwaka kwenye kiwango cha chini cha mshahara ni takwa la Sheria ya Viwango vya Chini vya Mishahara. Kiwango cha chini cha mshahara kinatumika bila kujali hali ya uhamiaji ya mfanyakazi. Ongezeko la kiwango cha chini cha mshahara litaakisi kiwango cha mfumuko wa bei kulingana na Kielezo cha Bei cha Mlaji (Consumer Price Index, CPI-W) kwa eneo la Seattle–Tacoma–Bellevue.
Kuanzia Januari 1, 2026, biashara zitawalipa wafanyakazi $21.30 kwa saa.
Sheria ya Viwango vya Chini vya Mishahara huweka kiwango cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi wanaofanya kazi ndani ya mipaka ya jiji. Kiwango cha chini cha mshahara cha sasa Seattle mwaka 2025 ni $20.76 kwa saa.
OLS itatuma kwa barua bango lililorekebishwa la sehemu ya kazi lenye taarifa kuhusu viwango vya kazi kwa mwaka 2026 kwa kila biashara yenye leseni ya biashara ya Seattle. Nakala ya bango la sehemu ya kazi kwa Kiingereza na tafsiri katika lugha nyingine 33 zitapatikana hivi karibuni. Jijasili kupata gazeti la OLS kwa ajili ya taarifa za hivi karibuni kuhusu viwango vya kazi vya Seattle kwenye OLS website.
- Msaada kwa biashara: kwa usaidizi wa bila malipo na wa binafsi kuhusu utekelezaji wa kiwango cha chini cha mshahara cha Seattle na viwango vingine vya kazi, piga simu 206-256-5297, au tuma barua pepe. business.laborstandards@seattle.gov au bofya hapa ili kujaza ombi la fomu ya mtandaoni.
- Msaada wa wafanyakazi na umma: kuuliza swali, kutoa malalamiko au kutoa taarifa, piga simu 206-256-5297, barua pepe workers.laborstandards@seattle.gov, au bofya hapa ili kujaza ombi la fomu ya mtandaoni.